IKULU YA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI

                 

       IDALA YA MSEMAJI WA RAIS  

              

TAARIFA YA MSIBA

MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI AMEPOKEA KWA SIMANZI KUBWA HABARI KUHUSU KIFO CHAKE MAMA MZAZI WA MHANGA WA DEMOKRASIA NCHINI BURUNDI KILICHOTOKEA TAREHE 27 JANUARI 2018.

MZAZI HUYO ALIYETUTOKA GHAFLA ALIKUWA MWENYE MOYO WA UPENDO, HURUMA NA FARAJA KUBWA KWA WATU WENGINE. HAYO YALIDHIHIRIKA KATIKA SIKU ZILIZOFUATIA KUUAWA KWAKE MWANAYE AMBAYE PIA ALIKUWA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI, HAYATI MELCHIOR NDADAYE.

MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI ANATOA SALAMU ZAKE ZA RAMBIRAMBI KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU, BILA KUSAHAU WAPENZI WA DEMOKRASIA NA WARUNDI WOTE WALIOANDAMANA NAYE HAYATI MELCHIOR NDADAYE AMBAYE ALIKUWA KWAO MFANO WA KUIGWA NA MWANGA USIOZIMIKA.

MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI ANATOA AGIZO LAKE KWA SERIKALI YA BURUNDI KUENDESHA MIKAKATI YOTE HUSIKA, ILI KUHAKIKISHA MZAZI HUYO ANAFANYIWAMAZISHI YA HESHIMA.

MHESHIMIWA RAIS PIERRE NKURUNZIZA, ANAPENDA KUSISITIZA KAULI YAKE ALIYOITOA TANGU MWAKA WA 2005 KWAMBA ATAENDELEA KUWA KARIBU YA FAMILIA YA HAYATI MELCHIOR NDADAYE NA KUISAIDIA KATIKA HALI NA MALI BILA KUCHOKA.

MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI ANAHITIMISHA KWA KUMWOMBA MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MZAZI THEREZA BANDUSHUBWENGE MAHALA PEMA PEPONI NA KUENDELEA KUWA MFARIJI WA FAMILIA YAKE DAIMA.                            

                                              Imetolewa jijini Bujumbura, tarehe  28/01/2018

                                                     J.C Karerwa Ndenzako      

                                                                                Msemaji wa Rais.-